Jinsi ya kuondoa sumu mwilini
Tambua ya kuwa unaweza kuwa na sumu nyingi mwilini. Usihofu!
Kwa nini tuwe na sumu mwilini?
Unafikiria kuwa una afya njema, lakini haujisikii vyema. Unapuuza, unaona ni vitu vidogo vidogo. Hivyo, haushughuliki kwenda hospitali au kwa wataalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu. Hatimaye tatizo linakuwa kubwa. Unafika hospitali unaambiwa una saratani, unapata mshtuko mkubwa! Unaambiwa chanzo cha ugonjwa hakifahamiki, ila unaelezwa chakula na mtindo wa maisha kwa ujumla ni sababu kubwa. Hii ina maana kuna uwezekano umeingiza sumu nyingi mwilini. Kinga ni bora kuliko tiba. Kama ungeelewa mapema, ungejikinga na saratani.
Sizungumzii sumu za kung'atwa na nyoka, wala sizungumzii sumu zinazohitaji matibabu ya dharura. Nazungumzia sumu ambazo zinatuua polepole na kimya kimya bila ya sisi kujua wala kutambua chochote. Nazungumzia sumu ambazo kila kuchapo tuko kwenye mlango wa daktari. Kila kuchapo afya zetu hizidi kuzorota zaidi. Hizi ni sumu ambazo ziko kwenye vyakula vyetu. Ni sumu tunazozivuta katika hewa kila siku kutokana na mioshi ya magari, viwanda n.k. Sumu ambazo zinaweza kutokana na madawa mbalimbali tunayojitibia afya zetu, sumu zinazotokana na vipodozi mbalimbali tunavyotumia kila siku kwa ajili ya urembo na kupendeza.
Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tuvute hewa, hata kwa sekunde kadhaa tusipopata hewa ya oksijeni tunakufa. Lakini tunavuta hewa iliyochafuliwa na mioshi ya viwanda na magari ambayo imetamalaki kila kona. Hivyo lazima tufe polepole na kimya kimya!
Tunapata sumu mwilini kwa sababu lazima tule na tunywe. Lakini kwa bahati mbaya, vyakula vingi tunavyokula siyo salama, vimesheheni kemikali.
Tunapata sumu kwa sababu lazima tujipodoe, lazima tujipambe tupambike, na lazima tung'are tupendeze. Kwa bahati mbaya sana, vipodozi vingi vimekuwa siyo vipodozi, ni vipopozi. Vimejaa kemikali ambazo huleta madhara mengi ya kiafya. Tunapongeza mamlaka ya chakula na dawa, TFDA, kwa kuviteketeza baadhi ya vipodozi na kutoa orodha ya vipodozi visivyofaa, lakini hata hivyo juhudi kubwa lazima ifanyike.
Ni kwa njia gani tunaingiza sumu mwilini?